Monday, 1 June 2015

TAKWIMU: KILA SIKU WATU WAWILI WANAUWAWA NA POLISI MAREKANI


Siku zote inaaminika kuwa Polisi ni chombo maalum chenye lengo la kuhakikisha usalama wa nchi, raia pamoja na mali zao, lakini huko nchini Marekani kuhusu hili la usalama wa raia lipo kinyume kidogo.

Kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa na gazeti la Washington Post zinaonyesha kuwa idadi ya watu wanaouawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa polisi nchini Marekani ni ya juu kuliko inavyodhaniwa. Polisi wanawaua watu wawili kila siku.

Gazeti hilo linasema kuwa wakati wa kipindi cha miezi mitano ya kwanza ya mwaka huu takriban watu 385 waliuawa ikiwa ni sawa na zaidi ya watu wawili kila siku. Huku Wanaume wakiwa 365 na wanawake 20.

Hata hivyo takwimu hizo zinaonesha kuwa idadi ya watu weusi ilikuwa ni ya juu mno hususani wale ambao hawakuwa na silaha yoyote. Marekani imeshuhudia visa kadha ambapo watu weusi wanauawa na polisi wazungu.

Takwimu hizo zimeonesha kuwa tangu mwaka wa 2008 watu 400 wanauawa kila mwaka na polisi. Pia kuulingana na takwimu hizo watu weusi wamo katika hatari mara tatu zaidi ya kuuawa na polisi.

Asilimia kubwa ya watu weusi waliouawa walikuwa wamejihami ijapokuwa mmoja kati ya 6 hawakuwa wamejihami ama walikuwa wamebeba bastola bandia.

Washington Post imekuwa ikifuatilia kwa karibu vifo vyote vilivyotokea mikononi mwa polisi tangu kuanza kwa mwaka huu wakifanya mahojiano na kunukuu ripoti za polisi na zile za vyombo vya habari mashinani.

Gazeti hilo pia limegundua kuwa kunatokea takriban vifo2.6 kila siku ikilinganishwa na takwimu ya serikali ya kifo cha mtu mmoja 1.1 kila siku kwa mujibu wa takwimu za idara ya upelelezi ya FBI.

No comments:

Post a Comment