Thursday, 18 June 2015

TENDE HUTUMIKA SANA KATIKA MFUNGO WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI, LEO ZIPO HAPA FAIDA ZAKE


Hapa nchini tende hupatikana kwa wingi kisiwani Zanzibar pamoja na Pemba, ambapo imekuwa kama ni sehemu ya chakula cha kiutamaduni visiwani humo.

Aidha tunda hili limekuwa likitajwa katika vitabu vitukufu vya dini, huku tunda hili likionekana kutumiwa sana na waumini wa dini ya Kiislamu hususani katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kama hiki tulichoanza leo.

Tunda hili limekuwa likitumika zaidi katika kipindi hiki kwasababu ya uwezo wake wa kurejesha nguvu mwilini kwa haraka zaidi.

Mtaalam wa tiba asili kutoka Mandai Herbalist Clinic, Dk Abdallah Mandai anasema kuwa tende ni chanzo kizuri cha virutubisho na nishati mwilini, lakini pia huuwezesha mwili kujipatia nguvu kwa haraka sana na hiyo ndio sababu ya tunda hili kutumika kwa wingi katika Mfungo wa Ramadhani, kwani waumini waliofunga hulitumia tunda hili ili kurudisha nguvu na nishati iliyopotea mchana kutwa walipokuwa wamefunga.

Aidha, Dk Mandai anaeleza kuwa ndani ya tende kuna virutubisho kama vile ‘calcium,’ ‘protein,’‘potassium,’‘magnesium,’ ‘phosphorous,’ ‘vitamin A’ ‘foliate’ na‘carbohydrates,’ ambazo zote kwa pamoja ni muhimu katika miili yetu kiafya.

Hata hivyo, mtaalam huyo anafafanua kuwa tende ni chakula cha afya na huwa na mkusanyikowa ‘vitamin A,’ ambayo husaidia katika kuongeza nuru ya macho.

Pia, ndani tende kuna madini ya ‘calcium,’ ambayo husaidia kuimarisha mifupa, hali kadhalika ndani ya tunda kuna‘vitamin B6’ na B12, ambazo husaidia katika usagaji na ufyonzaji mzuri wa chakula na kuingia katika mishipa ya damu.

Mbali na hayo, tende pia hutibu maradhi ya tumbo kama vile kujaa gesi, kuharisha na kuchafuka kwa tumbo, huku akibainisha kuwa pia tende husaidia kuondoa sumu mwilini na kusaidia kuongeza nguvu za kiume endapo litatumika kwa kufuata ushauri wa kitabibu.

Pamoja na hayo, tende ni tunda la pekee lenye uwezo wa kuupa mwili vitu vinne kwa wakati mmoja ambavyo ni protini, wanga,vitamin na mafuta. Pia ni tunda ambalo huyeyuka haraka sana tumboni, hivyo kutolipatia tumbo shida ya kufanya umeng’enyaji (digestion).

Pia anaeleza kuwa tende ni chakula bora kwa wanawake wanaonyonyesha kutokana na kusaidia kuyapa maziwa virutubisho muhimu ambavyo humfanya mtoto kuwa na afya bora.

Zaidi ya yote hayo, uwepo wa madini ya chuma ndani ya tende, husaidia kuwapa ahueni watu wenye upungufu wa damu mwilini. Hivyo basi, mbali nakupenda kutumia tende kipindi cha Mwezi wa Ramadhani tu, ni vizuri tukatumia siku zote kama jinsi tunavyotumia vyakula vingine, ili kuweza kuimarisha afya zetu kikamilifu.

Ikiwa unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo sugu ni vyema ukafanya uamuzi sahihi wa kufika Mandai Herbalist Clinic ili kuonana na Tabibu Abdallah Mandai na kuweza kupata matibabu sahihi. Unaweza kupiga simu namba; 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika moja kwa moja ofisini Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.  


No comments:

Post a Comment