Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 29 June 2015

UCHAGUZI WA WABUNGE WAFANYIKA NCHINI BURUNDI PAMOJA NA VYAMA PINZANI KUSUSA!!


Kuna ule usemi usemao ‘ukisusa wenzio wala’, hivyo ndivyo tunaweza kusema kwa sasa kutokana na hali ya huko nchini Burundi.

Unaweza sema hivyo kwa sababu pamoja na vyama vya upinzani na Umoja wa Afrika kususia uchaguzi wa nchi hiyo, bado nchi hiyo imefanya uchaguzi wa wabunge leo.

Hata hivyo, taarifa zinasema kuwa baadhi ya vituo vya kupigia kura vilifunguliwa kwa kuchelewa baada ya maguruneti kurushwa.

Wakati uchaguzi huo ukifanyika itakumbukwa kuwa vyama pinzani vya nchi hiyo vimetangaza kutoshiriki katika uchaguzi huo, halikadhalika pia Umoja wa Afrika umekataa kutoa waangalizi na kusema kuwa baadhi ya masharti yaliowekwa hayajaafikiwa kwa uchaguzi kuwa huru na haki.

Kimsingi yote hayo yanafuatiwa baada ya Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza kutaka kuwania muhula wa tatu.

Zaidi ya watu 70 wameuawa tangu mgogoro huo uanze.Karibu watu 130,000 wamelitoroka taifa hilo.

Shukrani kwa kuendela kuungana nasi mdau wetu, pia tunapenda kukukaribisha kutangaza biashara yako kupitia website hii, gharama zetu ni nafuu sana. Tupigie simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment