Advertisement

Advertisement

Shop

Shop

Mixer

Mixer

Friday, 26 June 2015

UFAHAMAMU UMUHIMU WA TUNDA LA MPESHENI


Habari za leo mpenzi msomaji wa tovuti yetu karibu katika muendelezo wa kupeana taarifa kuhusu mimea tiba na afya kwa ujumla.

Leo napenda tuzungumzie mapesheni, tunda hili mmea wake hukuwa kwa kutambaa, hivyo katika ukuaji wake ni muhimu kuweka miti ili iweze kusaidia kukua vizuri.

Mapesheni yanasifika kwa kuwa na virutubisho bora kwa afya ya binadamu ikiwemo vitamin A, C, B2, B6, na E, flavonoids, pectin pamoja na madini ya chuma.

Mpesheni yanauwezo mzuri katika kupunguza maumivu ya mishipa ya fahamu na maumivu ya tumbo la hedhi.

Halikadhalika hali mapesheni husaidia kutibu matatizo ya wasiwasi, msongo wa mawazo na hali ya kuzubaa kwa wazee na watoto.

Hata hivyo, watafiti wanasema kuwa, wajawazito na watoto wachanga wanapaswa kuchukua tahadhari wanapotumia tunda hili, hii ni kutokana na katika majaribio ya utafiti huo walibaini matunda hayo yanauwezo wa kusababisha uchungu na kusababisha watoto kuzaliwa kabla ya wakati, lakini pia huweza kusababisha usingizi hivyo si vizuri kutumiwa na madereva.

Ndugu yangu kama unateseka na magonjwa mbalimbali ni vyema ufanye utaratibu wa kuwahi kufika Mandai Herbalist Clinic sasa ili upate suluhisho la matatizo yako ya kiafya. Wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment