Thursday, 4 June 2015

UGONJWA WAZUKA KOREA KUSINI NA KUSABABISHA SHULE ZAIDI YA 700 KUFUNGWA.


Zaidi ya shule 700 Korea Kusini zimefungwa kuhofia kuenea kwa ugonjwa uliozuka ambao unaoshambulia mfumo wa upumuaji yaani Middle East Respiratory (MERS)

Kufuatia kuzuka kwa ugonjwa huo hadi sasa watu watatu wanadaiwa kufa, huku wengine 35 wakibakiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo.

MERS ni mara ya kwanza kugunduliwa nje ya Saudi Arabia, kwani miaka mitatu iliyopita mgonjwa wa kwanza aligunduliwa huko Mashariki ya Kati.

Aidha, Rais wa Korea Kusini Park Geun-Hye amehimiza jitihada zaidi za kukabiliana na ueneaji wa virusi vya ugonjwa huo.

Hata hivyo inaelezwa kuwa raia wa nchi hiyo wamekubwa na wasiwasi mkubwa kutokana na kuzuka kwa ugonjwa huo.

Shukrani kwa kuendelea kutembelea tovuti yetu kama ungependa kuwasiliana nasi kujua zaidi kuhusu huduma zetu za kitabibu tupigie simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Karibu.

No comments:

Post a Comment