Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 29 June 2015

UMOJA WA AFRIKA (AU) NA VYAMA VYA UPINZANI WAAMUA KUMSUSIA UCHAGUZI NKURUNZINZA


Sehemu ya wananchi wakiandamana kupinga uamuzi wa Rais Pierre Nkurunzinza kuwania muhula wa tatu. (Picha kwa hisani ya mtandao)
Kufuatia machafuko yanayoendelea nchini Burundi kutokana na Rais wa nchi hiyo, Pierre Nkurunzinza kuendelea kushikilia msimamo wake wa kuhitaji kuwania muhula wa tatu katika uchaguzi wa rais mwezi ujao Umoja wa Afrika umeamua kususia uchaguzi huo.

Kutokana na uamuzi huo Umoja wa Afrika umesema hautawapeleka waangalizi wake wa uchaguzi katika uchaguzi wa wabunge wa Burundi utakaofanyika leo Jumatatu kwa sababu masharti ya uchaguzi huru na wa haki hayajazingatiwa.

Rais Pierre Nkurunzinza
Mbali na Umoja wa Afrika kujiweka kando katika uchaguzi huo, pia vyama vya upinzani nchini humo navyo vimesusia uchaguzi, huku wakipinga uamuzi wa Rais Nkurunziza kugombea muhula wa tatu katika uchaguzi wa rais mwezi ujao.

Kitendo cha Rais Nkurunziza kuendelea kuhitaji kuwania muhula huo wa tatu kimesababisha wimbi la ghasia ambapo zaidi ya watu sabini wamepoteza maisha tayari.

Shukrani kwa kuendela kuungana nasi mdau wetu, pia tunapenda kukukaribisha kutangaza biashara yako kupitia website hii, gharama zetu ni nafuu sana. Tupigie simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment