Saturday, 6 June 2015

VIAZI MVIRINGO NI SULUHISHO LA MIGUU KUWAKA MOTO


Habari za Jumamosi ya leo mpendwa msomaji wetu, karibu katika mfululizo wetu wa kujuzana mambo mbalimbali.

Leo ningependa kukwambia kuhusu tatizo la miguu kuwaka moto na namna ya kulitibu tatizo hilo.

Tatizo hili mara nyingi huchangiwa na mzunguko dhaifu wa damu katika miguu na ukosefu wa virutubisho na madini yanayohitajika ndani ya mwili.

Unachopaswa kufanya ili kukabiliana na tatizo hilo ni rahisi sana tafuta viazi mviringo kisha fuata maelekezo haya yafuatayo:

Osha kwanza miguu yako kwa maji ya moto na sabuni, kisha jisuuze kwa maji ya baridi.

Kisha ponda viazi hadi viwe ujiuji kabisa kisha baadaye tumia ujiuji huo kupaka sehemu zote unazohisi zikiwaka moto.

Baada ya saa moja, osha miguu yako kwa maji baridi. Rudia tiba hii mara kwa mra kwa wiki kadhaa hadi pale utakapoona mabadiliko.

Unapofika Mandai Herbalist Clinic utapata dawa ya tatizo hili ambayo tayari imeshaandaliwa vizuri kabisa kwaajili yako na itamaliza tatizo lako la miguu kuwaka moto. Tupigie simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Karibu.

No comments:

Post a Comment