Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 30 June 2015

VIJANA SASA WAMEAMKA KATIKA SIASA KUNA HUYU MWINGINE LEO KATANGAZA NIA YAKE YA KUWATUMIKIA WAKAZI WA KATA BUNJU (DSM)Ikiwa tunaelekea katika uchaguzi mkuu wa viongozi mbalimbali nchini pale itakapofika mwezi Octoba mwaka huu vijana wameonekana kuwa na dhamira ya dhati katika kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi huo.

Suala la vijana kujitokeza katika safari ya kuwania nafasi mbalimbali ni jambo zuri na kutia moyo kwa taifa, huku likituacha tukiwa na imani kuwa tuna vijana wenye uwezo wa kuongoza nchi, lakini swali la msingi ni je, vijana hawa wataweza kulitoa taifa hili kwenye changamoto mbalimbali zilizopo kwa sasa?

Said Abdallah Mbonde yeye ni mmoja kati ya wale vijana wengi ambao huenda wanadhamira ya dhati ya kuwatumikia Watanzania.

Akizungumza na www.dkmandai.com Mbonde amesema amekusudia kugombea udiwani katika kata ya Bunju  na amejipanga kuwatumikia wananchi wa kata hiyo kwa hali na mali.

Aidha, akizungumzia vipaumbele vyake Mbonde amesema kuwa " kipaumbele cha kwanza kwa upande wa vijana ni michezo kwa sababu mimi na imani michezo ni afya, mtu akishiriki michezo akichoka si rahisi kufanya mambo ya ulevi na anasa."

Unaweza kusikiliza vipaumbele vingine vya kijana huyu Mbonde mwenye dhamira ya kuiongoza kata ya Bunju hapa chini. Bonyez Play hapa chini ili umsikilize mwenyewe...

No comments:

Post a Comment