Tuesday, 2 June 2015

WAANDAMANAJI WAAMUA KUANDAMANA WAKIWA UCHI NCHINI UGANDA


Waandamanaji wakiwa wamejilaza chini katika maandamano hayo Uganda

Tumekuwa tukishuhudia maandamano mbalimbali yakiwa na malengo ya kuishinikiza serikali kufanya baadhi ya vitu au kutofanya baadhi ya vitu. lakini haya ya uganda huenda yakawa ni maandamano ya aina yake kwa hiki walichoamua kukifanya waandamanaji hao.

Wanawake kutoka kijiji kimoja cha kazkazini mwa Uganda waliamua kuandamana wakiwa uchi kutokana na mgogoro wa ardhi kati ya utawala wa eneo hilo na jamii ambao umeendelea kwa takribani miaka 10.

Inaelezwa kuwa wakati wa maandamano hayo , mawaziri wa serikali na watafiti walipanga kukata kipande cha ardhi katika kijiji cha Apaa huko Amuru.


Maandamano wakiwa uchi nchini Uganda
Mwandishi wa BBC anasema kuwa katika kabila la Acholi, mwanamke anapovua nguo na kubaki uchi ni zaidi ya kupigana kwa kuwa kitendo hicho hutoa laana kwa mpinzani wake.

No comments:

Post a Comment