Wednesday, 24 June 2015

WAKATI DUNIA IKIWA IMEANZA KUSAHAU MACHUNGU YA UGONJWA WA EBOLA, LEO KUNA TAARIFA YA MLIPUKO WA UGONJWA HUO KUANZA UPYA

Mwaka 2014 haukuwa mwaka wenye taarifa nzuri kabisa hususani katika nchi za Afrika Magharibi kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, ugonjwa ambao ulisababisha vifo vya wa watu wengi katika mataifa hayo.

Lakini taarifa za matumaini za kupungua kwa mlipuko wa ugonjwa huo zilianza kutoka mwaka (2015) huu Januari, ambapo baadhi ya nchi kama Mali zilianza kutoa taarifa za kumalizika kabisa kwa ugonjwa huo hatari.

Sasa leo tena Juni 24, 2015 kuna hii taarifa ambayo si nzuri kwa nchi ya Sierra Leone ambapo mlipuko wa ugonjwa huo umeelezwa kuibuka upya.

Kwa mujibu wa Maofisa wa afya nchini Sierra Leone wamesema kwamba kuna wagonjwa wawili wapya wanaougua ugonjwa wa ebola na kwamba wamegunduliwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Freetown.

Hapo awali ilidhaniwa kwamba mji huo ulikuwa hauna maambukizi ya ugonjwa huo,na hakukuwa na wagonjwa walioripotiwa hapo kabla kwa muda wa wiki kadhaa.

Naye msemaji wa kituo cha karantini cha taifa hilo amesema kwamba kulikuwa na wasiwasi mkubwa kwasababu vituo vyote vya karantini na vitendea kazi vyake vilikuwa vimefungwa mjini Freetown.

Aidha, msemaji huyo akaongeza kusema kwamba kuna shaka kuwa kutatokea maambukizi mapya kutoka katika eneo lenye msongamano wa makazi duni.

Pamoja na hayo, nako upande wa Kaskazini mwa nchi hiyo ya Sierra Leone unaendelea kupata maambukizi mapya ya ugonjwa.

Kuhusu taarifa zetu za www.dkmandai.com au matangazo piga simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment