Thursday, 11 June 2015

WALIMU ZAIDI 100 WASIMAMISHWA KAZI NCHINI KENYA


Mwenyekiti wa Muungano wa Wazazi nchini Kenya Musau Ndunda
Tume ya huduma ya walimu nchini Kenya, imewafungia zaidi ya walimu mia moja kufuatia makosa mbalimbali ikiwemo udhalilishaji wa kijinsia.

Tume hiyo imesema kuwa imekuwa ikiwachunguza kwa makosa mbalimbali likiwemo hilo la uzalilishaji wa kijinsia, hivyo walimu hao kwa sasa wameondolewa usajili rasmi wa walimu na hawatoruhusiwa kurejea kufundisha nchini humo.

Taarifa iliyopatikana kwenye gazeti la serikali ya Kenya, imesema kuwa tume ya huduma ya walimu imetoa majina ya walimu 126, huku walimu wawili kati yao waliofukuzwa kazi ni wanawake.

Pia taarifa hiyo inasema kuwa walimu hao walifukuzwa kazi baada kupitia mchakato wa kinidhamu ambao umewakuta na hatia ya makosa mbalimbali.

Aidha, taarifa hiyo ilionya kwamba, kama mwalimu yeyote kati ya waliofungiwa atadharau uamuzi huo, basi atapigwa faini ya hadi kufikia dola za Kimarekani 50 au kifungo kisichozidi miezi sita au vyote viwili.

Miaka ya hivi karibuni kumekuwepo na ongezeko la idadi ya walimu ambao wamekuwa wakituhumiwa kwa tabia chafu huku baadhi yao wakihusika kuwadhalilisha wanafunzi kijinsia.

Miongoni mwa matukio ya kidhalilishaji ni pamoja na lile la mwalimu mkuu huko Nyaza ambaye alikamatwa na polisi baada kumvua nguo mwanafunzi wa kike kwa sababu alivaa sketi fupi. Mwalimu huyo anaendelea kushikiliwa na poliosi.

Nao Umoja wa walimu wa shule za msingi nchini Kenya umeelezea msimamo wake kwamba hawatomlinda mwanachama yeyote atakayekiuka maadili. Mwenyekiti wa muungano wa wazazi nchini Kenya Musau Ndunda ameitaka tume ya walimu kuwachunguza walimu wote ili kuzuia watoto wadogo kudhalilishwa kijinsia.

Endelea kuwa karibu nasi kwa taarifa mbalimbali kutoka tovuti hii ya www.dkmandai.com, lakini inapofika wakati utajisikia haupo vizuri kutokana na kuumwa basi wasiliana nasi Mandai Herbalist Clinic  kwa simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Karibu. 

No comments:

Post a Comment