Thursday, 25 June 2015

WANAFUNZI WAMEBUNI HIZI KONDOMU ZENYE UWEZO WA KUTAMBUA MAGONJWA YA ZINAA


Wanafunzi katika shule moja nchini Uingereza wameunda mipira ya kondomu inayowaonya watumiaji wanapojamiana na mtu aliyeambukizwa maradhi ya zinaa.

Kondomu hiyo inabadili rangi pindi inapokutana na majimaji ya mtu anayeugua maradhi ya zinaa.

Kondomu hiyo S.T.EYE inaweza kutambua maambukizi ya Chlamydia Kaswende na Kisonono.

Kulingana na wanafunzi hao kondomu hiyo inabadili rangi tofauti kulingana na bakteria iliyopo.

Uvumbuzi huu ni wa Daanyaal Ali, 14, Muaz Nawaz, 13 na Chirag Shah, 14, ambao ni wanafunzi katika shule ya Isaac Newton Academy iliyoko Ilford, Essex, nchini Uingereza.

''Tuliazimia kumpa onyo mtumiaji wa mipira hii kuwa mpenzi wake yuko salama ama ni mgonjwa bila ya wasiwasi wa kupimwa hospitalini''.


Wanafunzi hao tayari wametunukiwa, tuzo la ubunifu la ''the TeenTech'' .

Daanyall alisema kuwa "Walizindua kondomu hiyo ili kukifaidisha kizazi kijacho''
Pamoja na hayo, wavumbuzi hao wanasema kuwa hiyo ni mojawepo ya njia salama ya kubaini usalama penzi lenu.

 Kuhusu taarifa zetu za www.dkmandai.com au matangazo piga simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment