Wednesday, 10 June 2015

WANAWAKE WAANDAMANA KWA KUKOSA WAUME WA KUWAPA UJAUZITO KENYA


Taarifa za wanawake kulalamika kutokana na wenzi wao kushindwa kuwatimizia mahitaji ya kindoa kwasababu ya ulevi ni moja ya stori ambazo zilisikika sana hapa nchini mwezi uliopita kutoka Rombo.

Lakini leo kuna hii stori kutoka nchini Kenya ambapo wanawake katika jimbo la Ndeiya nao wamelalamika kutokana na waume zao kushindwa kuwapa ujauzito kutokana na mwenendo wa unywaji wa pombe haramu ambazo zinaathiri nguvu za kiume.

Wanawake hao kutoka Kenya wao waliamua kuandamana kabisa ili kuonesha wamekwazika na tatizo hilo, ambapo inaelezwa kuwa maandamano hayo yalikuwa ni ya amani na yalifanyika katika kituo cha biashara cha Thigio.

Mmoja miongoni mwa wanawake waliokuwa wakiandamana alifahamisha kuwa iwapo tabia hiyo ya ulevi haitorekebishwa basi itawalazimu kutoka nje ya ndoa zao na bila wao kujua lolote na kuwahudumia watoto wasiokuwa wao.

Nancy Wangare alifahamisha kuwa katika kijiji hicho wanawake wachache walioolewa wamevumilia kwa kiasi kikubwa kutokana na upungufu wa nguvu za kiume kwa waume zao kutokana na pombe wanazokunywa.

Asante kwa kuendelea kuwa karibu nasi na kuendelea kupata taarifa mbalimbali kutoka kwetu, lakini kumbuka kuwa ikiwa unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali likiwemo tatizo la nguvu za kiume pia, basi fika Mandai Herbalist Clinic utapata matibabu sahihi kwa kutumia tiba zitokanazo na mimea, matunda, nafaka na mitishamba kutoka kwa Dk. Abdallah Mandai.

Tupigie simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe,dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Karibu.

No comments:

Post a Comment