Tuesday, 9 June 2015

WATAWA WAWILI WAKWAMA KWENYE LIFTI WAKAA SIKU TATU BILA KULA WALA KUNYWA


Hivi ni mara ngapi umewahi kukwama kwenye lifti? na unakumbuka ilikuchukua muda gani hadi kupata msaada wa kutolewa?

Huenda wewe ukawa ni miongoni mwa watu ambao wamewahi kukwama kwenye lifti nakujikuta katika wakati mgumu, lakini watawa hawa wawili kutoka mjini Rome wao huenda walikutwa na wakati mgumu zaidi kwani wao walikwama kwenye lifti na kukaa humo bila kula wala kunywa ndani ya siku tatu.

Watawa hao mmoja mwenye umri wa miaka 69 raia wa New Zealand na mwingine wa miaka 58 raia wa Ireland walikwama ndani ya lifti hiyo siku ya Ijumaa baada ya kutokea kwa hitilafu ya umeme.

Inaelezwa kuwa baada  ya kukwama siku hiyo ya Ijumaa wakaja kugunduliwa siku ya Jumatatu wakati mfanyakazi mmoja alipokosa kujibiwa baada ya kubonyeza kengele ya mlango na akaamua kuwaita polisi

Wakati polisi walipoingia kwenye nyumba hiyo, waliita kutaka kujua ikiwa kulikuwa na mtu ndipo watawa hao wakaitika wakisema kuwa wako ndani ya lifti.

Walipotolewa walisema kuwa waliomba sana. Kisha walipelekwa hospitali iliyo karibu ambapo walipata matibabu.

Endelea kuwa karibu nasi kwa taarifa mbalimbali kutoka tovuti hii ya www.dkmandai.com, lakini inapofika wakati utajisikia haupo vizuri kutokana na kuumwa basi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Karibu.

No comments:

Post a Comment