Saturday, 13 June 2015

WATU MILION 400 HAWAPATI HUDUMA ZA AFYA DUNIANI


Ripoti mpya ya Shirika la Afya duniani WHO na Benki ya Dunia imeonesha kwamba watu milioni 400 duniani kote bado hawapati huduma za msingi za afya.

Ripoti hiyo pia imebainisha kuwa asilimia sita ya watu wanaopatikana kwenye nchi zenye kipato cha chini au cha wastani wanasukumwa kwenye dibwi la umasikini kwa sababu ya matumizi ya fedha nyingi zaidi kwenye afya.

Ripoti hiyo imeangalia upatikanaji wa huduma zote za afya zikiwemo mpango wa uzazi, huduma za wanawake wajawazito, chanjo kwa watoto, dawa za kupunguza makali ya ukimwi, ARV, dawa za kutibu kifua kikuu na upatikanaji wa mafi safi na kujisafi kwa mwaka 2013.

Akihojiwa na redio ya Umoja wa Mataifa, Tessa Tan Torres Edejer, Mratibu wa Maswala ya mifumo ya afya wa WHO, ameeleza kwamba sababu ya kwanza ya kukosa huduma za msingi ni umaskini.

" Hawapati huduma hizo kwa sababu hawana pesa ya kutosha kwa matibabu watakayopaswa kulipa, mfano dawa au chanjo."
Sababu nyingine ni kwamba, hata kama vituo vya afya vipo, huenda havina dawa au wafanyakazi kuwahudumia.

Naye Marie-Paule Kieny, Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu wa WHO, amesema serikali zinapaswa kuwapatia huduma za afya watu maskini zaidi, wanawake na watoto, wale wanaoishi mbali.

Halikadhalika WHO na Benki ya Dunia zimependekeza serikali zinazotaka kutekeleza huduma za afya kwa wote zilenge angalau asilimia 80 ya watu.

Pia mashirika hayo yamesema kuwa ripoti nyingine kama hizo zitatolewa kila mwaka, ili kutathimini mafanikio ya nchi katika kufikisha huduma za afya kwa wote.
  
Endelea kuwa karibu nasi kwa taarifa mbalimbali kutoka tovuti hii ya www.dkmandai.com, lakini inapofika wakati utajisikia haupo vizuri kutokana na kuumwa basi wasiliana nasi Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Karibu. 

No comments:

Post a Comment