Monday, 8 June 2015

YAFAHAMU MAMBO MUHIMU WAKATI WA KIPINDI CHA UJAUZITO
Wakati wa ujauzito ni wakati ambao mama mjamzito hupaswa kuwa makini kwa kila kitu hususani kuhusu afya yake.

Moja ya mambo ambayo mama mjamzito hupaswa kuzingatia katika kipindi hicho ni pamoja na kula vyakula vyenye virutubisho vya kutosha pamoja na madini ya chuma, hii ni kwa sababu madini hayo ya chuma husaidia kuongeza damu mwilini na hivyo kumsaidia mwanamke pale anapokuwa amepoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.

Aidha, mama mjamzito pia anapaswa kuepuka maambukizo katika mlango wa kizazi na sehemu za siri na endapo itatokea maambukizi ni vyema akapata matibabu sahihi mapema zaidi.

Pia mama mjamzito anapaswa kuepuka matumizi ya pombe na dawa za kulevya, matumizi ya vilevi hivyo huhatarisha afya ya mtoto na huweza kuchangia mtoto kuzaliwa akiwa na ulemavu, hivyo wataalam wa afya hupendekeza mama mjamzito asinywe pombe hata kwa kiwango kidogo.

Halikadhalika mama mjamzito hupaswa kuepuka kutumia dawa hovyo pasipo kupata maelekezo maalum ya daktari.

Mbali na hayo, pia mama mjamzito anatakiwa kuepuka kuwa na uzito kupita kiasi pamoja na kuzingatia usafi wake binafsi ambao ni wa kawaida tu kama vile kudumisha kunawa mikono na kuosha vyakula kabla ya kula.

Unaweza kuwasilina nasi kwa namba za simu zifuatazo 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Karibu.


No comments:

Post a Comment