Wednesday, 29 July 2015

BAADA YA ACT- WAZALENDO KUTANGAZA KUTOJIUNGA NA UKAWA CHAMA CHA TLP NAO WAMETOA MAAMUZI YAO HAPA

Chama cha TLP kimesema hakipo tayari kuungana na chama kingine chochote kile kwa makubaliano ya kumsimamisha mgombea mmoja badala yake kitasimamisha mgombea wake makini ambaye ataingia katika kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya urais.

Kauli hiyo imetolewa na naibu katibu mkuu wa chama cha TLP taifa Dominata Rwechungura wakati akiongea na wananchi wa kata ya Kishogo wilayani Bukoba ambapo amewataka watanzania kuendelea kuwa na imani na chama hicho na akawasisitiza wananchi kutowasikiliza wanasiasa wanaopanda kwenye majukwaa na kuwarubuni.

Katika hatua nyingine Rwechungura amewataka watanzania ili kutokubali  kununuliwa kwa gharama nafuu na wanasiasa wanaopitisha pesa kwa wananchi ili waweze kuchaguliwa hali ambayo inaweza kusababisha kupata viongozi wabovu wasio na sifa ya kuliongoza taifa.

Endelea kuwa karibu na tovuti hii kwa taarifa zaidi kila siku, lakini pia unaweza kutangaza nasi kwa gharama nafuu sana tupigie simu namba 0716 300 200, 0784 300 300

No comments:

Post a Comment