Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 7 July 2015

BAADA YA KUITUMIKIA VYEMA MANISPAA YA ILALA KAMA MEYA SASA JERRY SILAA AOMBA RIDHAA YA KUGOMBEA UBUNGE


Jerry Silaa
Tarehe 6, Julai, 2015 ndio tunaweza kusema ilikuwa siku ya mwisho au kuvunjwa kwa baraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na kuahirishwa kwa vikao mpaka baada ya uchaguzi Mkuu.

Kupitia Mkutano huo Jerry Silaa alitangaza kuvua madaraka ya umeya na kugombea nafasi ya ubunge wa jimbo la Ukonga 2015 .

Akizungumzia uamuzi wake huo wa kugombea nafasi hiyo ya Ubunge Silaa alisema "nimeamua kwa dhati kabisa kuomba Ubunge kwenye jimbo la Ukonga, naomba wananchi wenzangu wanichague moja mimi nagombea Ubunge, la pili wanichague wanaCCM wenzangu kwa kuniamini kwamba chama chetu kikinichagua mimi kwa sifa na uongozi niliyoufanya kwa zaidi ya nusu ya uhai wangu tunaweza tukashinda uchaguzi unaokuja"

Aidha Silaa aliongeza kuwa "mimi nikiwa mbunge wa Ukonga nitaisemea Ukonga, nitaisemea Ilala, nitaisemea Dar es Salaam na nitahakikisha Dar es Salaama inapata maendeleo endelevu"
Mbali na hayo Silaa pia amezungumzia mikakati yake katika kupunguza misongamano na matukio ya uhalifu jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa, "hii misongamano ya magari inayoonekana ni matokeo ya uwekezaji mdogo ya miundombinu Dar es Salaam, haya matokeo ya uhalifu ni matokeo usimamizi mdogo wa sheria na idadi ndogo ya Askari waliopo Dar es Salaam. Kazi hii sio ya Halmashauri, kazi hii sio ya Manispaa, kazi hii ni ya Serikali kuu kwa hiyo nadhani sasa tunahitaji watu wa kwenda kusema jinsi gani Dar es Salaam inapaswa kuendeshwa"

Pamoja na hayo alielezea kuhusu nafasi aliyokuwa nayo hapo awali kama Mstahiki Meya ambapo amesema kuwa "nimehudumu kama mstahiki meya manispaa kwa miaka mitano nafasi ya halmashauri ilikuwa ni kubwa nimemaliza salama mafanikio ni makubwa halmashauri leo hii ni kioo cha Dar es Salaam."

 Kama unahitaji kutangaza nasi kupitia tovuti hii, wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 80, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.Gharama zetu ni rahisi sana na tangazo lako litawafikia au kutazamwa na zaidi ya watu elfu themanini

No comments:

Post a Comment