Friday, 31 July 2015

BAADA YA WAKAZI WA DAR KUJITOKEZA KWA WINGI KATIKA UANDIKISHAJI WA WAPIGA KURA, NEC IMEAMUA KUFANYA MAAMUZI HAYA

Leo Julai 3, 2015 ndio ilikuwa iwe siku ya mwisho ya kukamirisha zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kwenye daftari la kudumu la wapiga kura (BVR) kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.

Zoezi la uandikishaji huo limeonekana kuwa na muitikio mzuri kwa wakazi wa jiji hilo, hivyo Tume ya Uchaguzi (NEC) imeamua kutangaza kuongeza siku nne zaidi za uandikishaji wa wapigakura kwa kutumia teknolojia ya BVR.

Kufuatia kuongezwa kwa siku hizo nne kutafanya zoezi hilo kuendelea hadi Agosti 4, mwaka huu ili kukabiliana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza kujiandikisha.

Hadi jana, zaidi ya wakazi 1,000,000 walikuwa wamekwishaandikishwa jijini Dar es Salaam, Huku Nec ikinatarajia kuandikisha jumla ya wakazi zaidi ya 2.8 milioni kwa jiji hilo lenye idadi kubwa ya watu nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Nec, Jaji Damian Lubuva, hadi sasa jumla ya zaidi ya watu 18 milioni wamekwishajiandikisha wakati tume ilitarajia kuandikisha watu kati ya 22 milioni na 23 milioni.

Unaweza kutangaza na tovuti hii sasa wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment