Wednesday, 8 July 2015

BRAZIL IMEDHAMIRIA KUPUNGUZA UZAZI WA UPASUAJISheria mpya nchini Brazil zinawalazimu madaktari kuwaarifu wanawake kuhusu hatari zilizopo na pia kuwashurutisha watie saini fomu za idhini yao kabla ya kuwafanyia upasuaji huo wakati wa kujifungua.

Madaktari hao pia watahitajika kutoa rekodi ya kujifungua kwa akina mama na kubainisha ni kwanini ilibidi wafanyie upasuaji.

Aidha, katika hospitali za umma wanawake  huona ndio njia salama na kwa walio na uwezo, wao huamua kuwalipa madaktari kando, kukwepa kukabiliwa na saa kadhaa za uchungu wa uzazi katika hospitali zilizo jaa wagonjwa.

Wanawake wengi Brazil hupendelea kuzaa kupitia upasuaji, hivyo wanawake walio tajiri wanaokwenda katika hospitali za kibinafsi, wanaona upasuaji wakati wa uzazi ndio njia ya kisasa ya kujifungua.

 Kama unahitaji kutangaza nasi kupitia tovuti hii, wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 80, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.Gharama zetu ni rahisi sana na tangazo lako litawafikia au kutazamwa na zaidi ya watu elfu themanini

No comments:

Post a Comment