Wednesday, 29 July 2015

CCM NAO WAMEFANYA MKUTANO LEO JULAI 29 ISHU YA LOWASSA KUHAMA NAYO ILIULIZIWA NA MAJIBU YAKE YAKATOLEWA YAPO HAPA!


Mwenezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam ndugu Juma Simba Gaddafi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)

Ikiwa ni siku moja tu tangu aliyekuwa Waziri Mkuu Mhe: Edward Lowassa kufanya maamuzi ya kukihama chama chake (CCM) na kuhamia CHADEMA leo Julai 29 CCM nao walikuwa na mkutano na waandishi wa habari mengi yamezungumzwa ikiwemo ishu hiyo ya Mh; Lowassa.

Katika mkutano huo Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba Gaddafi ndiye aliyefika na kuzungumza, huku Mkutano huo ukifanyika Peacock Hotel Dar, na si Makao Makuu madogo kama ilivyotangazwa jana.

Miongoni mwa maswali aliyoulizwa ilikuwa ni pamoja na suala la Lowassa kuhamia CHADEMA ambapo majibu ya Juma Simba Gaddafi yalikuwa hivi “Yeye aliingia CCM kwa ridhaa yake hakuna mtu alimlazimisha, ametoka kwa ridhaa yake na CCM itabaki kuwa CCM… Wafuasi walikuwa ndani ya CCM, kuondoka kwake ameondoka yeye na sio wa kwanza kuondoka”
Aidha akieleza zaidi kuhusu suala hilo Gaddafi amesema kuwa "Mtu akitoka huwezi kujibu kwa nini ametoka, nawathibitishia mtu yoyote akitoka CCM itabaki imara… Tutashinda asubuhi kweupe… Kama Lowassa angekuwa anaondoka na watu wengi ungewaona jana, lakini alikwenda yeye akarudisha kadi… watu wengi wanatoka kwenye Chama na CCM bado iko imara.'

Mbali na hayo, Gaddafi ametoa shukrani kwa ushirikiano waliopata katika Mkutano Mkuu

“CCM inatoa shukrani kwa ushirikiano mlioutoa katika Mkutano wetu Mkuu wa Kumtambulisha Mgombea Urais Dk. Magufuli pale Mbagala, CCM ni Chama chenye busara tumeona tuwashukuru”
Halikadharika Gaddafia amewashukuru waliojitokeza kugombea nafasi mbalimbali za ubunge na kuwataka wajitokeze kwa wingi pia kupiga kura.

"Kingine tunawashukuru waliojitokeza Kugombea nafasi mbalimbali za Ubunge na wajitokeze kwa wingi pia kupiga kura… Tumemaliza Uchaguzi Dodoma na kumpata Mgombea wetu Dk. Magufuli, tunajivunia kwa sababu ana rekodi nzuri… Tuna imani CCM itaendelea kuongoza 2015 mpaka 2020, tumefanya mengi yanayokubalika".


Unaweza kutangaza na tovuti hii sasa wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment