Thursday, 9 July 2015

DK. MANDAI ANAKUFAHAMISHA NAMNA MTI WA MBUYU UNAVYOWEZA KUKUTIBU MAGONJWA MENGI KWA WAKATI MMOJA


Dk. Abdallah Mandai akielezea namna mti wa mbuyu unavyoweza kuwa tiba

Mwenyezi Mungu katujalia miti mingi hapa duniani ambayo mingine imekuwa ni tiba nzuri sana kwetu binadaam dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Moja ya miti ambayo hupatikana hapa nchini nchini Tanzania ni pamoja na mbuyu. Mbuyu ni kati ya miti mikubwa na minene ambayo hupatikana katika ukanda wa tropiki.

Mazao ya mti huu hufahamika kama mabuyu, huku gamba la tunda hilo likiitwa kibuyu na ubuyu ni nyama ya tunda.
Mti wa mbuya
Mti huu umesheheni malighafi nyingi na nzuri katika afya ya binadamu, ambapo inaelezwa unga wa ubuyu huwa na vitamin na madini mengi, kwani unga huo una kiasi kingi cha vitamin C kushinda ile inayopatikana kwenye chungwa.

Dk Abdallah Mandai ni mtaalam wa mimea tiba kutoka Mandai Herbalist Clinic anasema kuwa mti huo wa mbuyu huweza kusaidia kutibu homa.

Dk. Mandai anasema il mti huo uweze kutumika kama tiba mgonjwa anapaswa kutafuta magome ya mti huo kisha kuyachemsha vizuri.

Ubuyu baada ya kuvunwa
Aidha, Dk Mandai anaeleza kwamba mti huo unauwezo wa kutibu ugonjwa wa malaria, kifua kikuu pamoja na pumu pale magome yake yanapotumika mara baada ya kuchemshwa.

Mbali na hayo, Dk Mandai anafafanua kuwa kwa wale wenye shida ya kikohozi wanapaswa kuchanganya unga wa tunda lake pamoja na asali kisha mgonjwa atalamba au kutumia kwa kuchanganja na maji ya moto.

Kama unahitaji ushauri au unamaoni zaidi unaweza kupiga simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.No comments:

Post a Comment