Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 23 July 2015

DK. MANDAI: MATUMIZI YA ASALI KWA WENYE HIV NI MUHIMU


Tabibu wa Tiba asili. Abdallah Mandai
Ugonjwa wa Ukimwi ni moja kati ya magonjwa hatari hapa nchinia na duniani kwa ujumla. Ugonjwa huu ni hatari kwa sababu tangu kugundulika kwake zaidi ya miongo mitatu iliyopita.

Ugonjwa huu hauna dawa hadi sasa na wataalam wamekuwa wakiendelea kuumiza vichwa ili kupata ufumbuzi wa ugonjwa huu, lakini kwa sasa zipo dawa ambazo husaidia tu kupunguza makali ya ugonjwa huu.

Tabibu wa tiba mbadala kutoka Mandai Herbalist Clinic, Dk. Abdallah Mandai anasema kwaamba virusi vya ugonjwa huo hurutubishwa na kupunguzwa nguvu kutokana na vyakula anavyokula mgonjwa husika.

Dk. Mandai anaeleza kuwa ugonjwa huo unaharibu kinga ya mwili hivyo husababisha mgonjwa kudhohofika kimwili.
Asali
Dk. Mandai anafafanua kuwa asali ni nzuri sana katika kupambana na ugonjwa huo na mengine mengi na anasema ni vyema asali ikatumika kama sukari katika chai itumike kama chakula au siagi katika mkate au mgonjwa anaweza kuitumia kwa kuilamba.

“Asali ni nzuri sana kwa watu wote hata kwa wasioathirika , pia ni kinga nzuri sana kwa magonjwa mbalimbali.” Anasema Dk. Mandai.

Aidha, Dk. Mandai anasema kuwa mtu ambaye hutumia asali mara kwa mara hujiweka katika nafasi nzuri ya kuepuka magonjwa mbalimbali, lakini pia ni tiba nzuri ya vidonda.

Mbali na hayo Dk. Mandai anasema kuwa chakula kingine kinachoweza kumweka vizuri mtu mwenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi ni pamoja na soya na alovera.

Ushauri

Ni vyema kupata ushauri kwanza kwa Tabibu Abdallah Mandai kabla ya kutumia tiba hii katika kuongeza kinga za mwili, lakini pia ni vyema tukakumbuka kuwa Ukimwi bado upon a unaua hivyo ni vyema kila mtu akawa makini kwa kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu na waliopima au kutumia kinga kila unaposhiriki tendo moja.

No comments:

Post a Comment