Wednesday, 8 July 2015

FAHAMU NAMNA MAJANI YA NANASI YANAVYOWEZA KUTIBU MAGONJWA


Habari za siku hii ya leo mpendwa mfuatiliaji wetu wa www.dkmandai.com leo ni siku nzuri tena ambapo tunaendelea kufahamishana kuhusu mimea tiba mbalimbali.

Kama umekuwa ukifuatilia tovuti hii naamini utakuwa unafahamu kwamba mara kadhaa tumeshazungumzia umuhimu wa matumizi ya tunda la nanasi kiafya.

Lakini leo Mandai Herbalist Clinic tunakufahamisha matumizi ya majani au matawi ya mmea wenyewe wa nanasi.

Majani haya yanauwezo wa kuwasaidia sana wale wenye matatizo ya figo, kujaa kwa miguu au miguu kuwaka moto na kupasuka.
Majani ya nanasi yakiwa tayari yamesagwa
Majani haya pia yanauwezo wa kuwasaidia wale wenye shida ya kuumwa na kichwa mara kwa mara.

Unachopaswa kufanya ili majani haya yawe msaada kwako ni kuhakikisaha unapata majani matano ya mmea huu wa nanasi kisha yasage na kuchanganya kwenye maji ya moto na baadaye chuja.

Baada ya hapo subiri maji hayo yenye mchanganyiko wa majani ya nanasi yapoe kisha mhusika yaani mgonjwa atumie kwa kunywa asubuhi mchana na jioni.

Kama unahitaji ushauri au unamaoni zaidi unaweza kupiga simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment