Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 21 July 2015

FAHAMU NAMNA VIAZI VYEKUNDU VINAVYOWEZA KUKUSAIDIA KUPUNGUZA SHINIKIZO LA DAMU


Viazi vyekundu ambavyo hujulikana pia kama ‘beetroots’ kwa lugha ya kiingereza hivi ni viazi vya mimea aina ya ‘beets’, huwa na rangi nyekundu vingine vikiwa njano au vyeupe.

Viazi hivi vinaelezwa kuwa na madini ya ‘nitrate’ ambayo husaidia kutanua na kulainisha mishipa ya damu, hivyo kupunguza shinikizo la damu na pia huimarisha kuta za ndani za mishipa ya damu.

Unaweza ukatumia viazi vyekundu kama juisi ya kusaga,unaweza kunywa glasi moja ya juisi ya viazi vyekundu kila siku peke yake au zaidi ya glasi moja kila siku kama ukiwa umechanganya na matunda mengine.

Juisi ya viazi vyekundu
Viazi hivi vyekundu vina madini ya potasiamu, chuma, vitamini A, B6 na C, asidi ya foliki, protini na wanga.

Pamoja na kusaidia kupunguza shinikizo la damu , faida nyingine za viazi vyekundu ni husaidia kuongeza damu mwilini na kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo na kuboresha mzunguko wa damu kwenye ubongo hasa kwa wazee.

Kwa maelekezo zaidi unaweza kuwasiliana na Dk. Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment