Friday, 3 July 2015

FAHAMU VIASHIRIA VYA FANGASI SEHEMU ZA SIRI

Fangasi ya ukeni husababishwa na fangasi aina ya Candida albicans. Ugonjwa huu huitwa vaginal candidiasis kwa kiingereza na ni kati ya magonjwa ambayo huwasumbua wanawake wengi mara kwa mara.

Fangasi hzi huambukizwa kwa njia ya kutumia vyoo vichafu pamoja na kuchangia nguo za ndani na taulo.

Joto kali na unyevunyevu mwingi pamoja na kuvaa nguo za kubana huchangia pia kutokea kwa fangasi ukeni. Ugonjwa huu unaweza kuambukizwa kwa njia ya ngono.

Viashiria au dalili za ugonjwa huu ni pamoja na kutokwa na maji maji meupe mfano wa maziwa kwenye uke, ambayo hayana harufu mbaya, pia mhusika huweza kuhisi kuwashwa sehemu za siri hasa kwenye uke na mashavu ya uke.

Dalili nyinginezo ni kupata maumivu wakati wa kukojoa kwa baadhi ya wagonjwa. Mara chache hali hii hutokea, jambo ambalo husababishwa na kuchubuka wakati wa kujiwasha.

Umnapohisi unatatizo hilo ni vyema ukaonana na wataalam wa afya kwa ajili ya uchinguzi zaidi kabla ya kupata matibabu.

Pamoja na hayo, ili kuepukana na tatizo hili ni vyema kuzingatia usafi wa nguo za ndani kwa kuvaa nguo safi zilizofuliwa vizuri na kuanikwa juani (au kupigwa pasi).

Pia hakikisha unavaa nguo za ndani zilizokauka vizuri. Epuka kuvaa zile zenye unyevunyevu au mbichi.

Mbali na hayo, pia ni vizuri ukazingatia usafi wa sehemu za siri na kujikausha vizuri mara baada ya kuoga. Huku pia usafi wa choo ukizingatiwa na kuimarishwa.

Pia unaweza kufika kwetu Mandai Herbal Clinic tukakupatia dawa nzuri ambayo itakusaidia kumaliza kabisa tatizo hilo hata kama unasumbuliwa na fangasi sugu. Jambo zuri zaidi kuhusu dawa zetu ni kwamba zimetengenezwa kwa mchanganyiko wa mimea asilia ambayo husaidia kuondosha tatizo hilo kabisa.

Tunapatikana Ukonga, Mombasa jijini Dar es Salaam. Au wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo: 0716 300 200, 0769 400 80, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment