Friday, 17 July 2015

FAHAMU VISABABISHI VYA UNENE, MADHARA YAKE NA NAMNA YA KUKABILIANA NA UNENE KUPITA KIASIKuna mambo mengi yanayoweza kuchangia mtu akawa mnene, lakini sababu nyingi husababishwa na mtindo wa maisha ikiwemo vyakula tunavyokula.

Miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na kutofanya mazoezi, kula vyakula vingi vyenye sukari na vyakula vyenye wanga, lakini baadhi yao huwa wanene kwasababu za kurithi.

Hata hivyo unaweza kupunguza unene kwa kutumia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya mzoezi mara kwa mara, kula matunda na mboga mboga kwa wingi na kuepuka matumizi ya vyakula na vinywaji vyenye sukari nyingi n.k.

Kimsingi tatizo hili la unene kupita kaisi huwa na madhara mengi kiafya na kijamii na hata kiuchumi. Baadhi ya madhara yanayoweza kusababishwa na unene uliopitiliza ni pamoja na matatizo ya moyo, shinikizo la damu, kukoroma kupita kiasi, kiarusi pamoja na kusababisha hatari ya matatizo ya uzazi kwa baadhi ya watu.

Karibu utangaze nasi sasa wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.Gharama zetu ni rahisi sana na tangazo lako litawafikia au kutazamwa na zaidi ya watu elfu tisini.

No comments:

Post a Comment