Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 10 July 2015

HAYA NDIYO ALIYOYASEMA RAIS KIKWETE KUHUSU TIMU YA TAIFA KUFUNGWA FUNGWA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amesema aliacha kwenda uwanjani kuiangalia timu ya taifa Stars kwa kuwa alionekana kuitia mkosi wa kufungwa timu hiyo kila ilipocheza

Hayo aliyasema wakati wa kulihairisha bunge na kuwaaga wabunge, ambapo Rais Kikwete alisema zamani alihudhuria sana mechi za Stars na baada ya kuwa inafungwa, aliamua kutokwenda uwanjani

“Mwanzoni nilikuwa navaa hadi jezi kuishangilia timu yetu ilipokuwa inafanya vizuri, tulipoanza kufungwa fungwa wakasema mzee unaitia timu mkosi, nikaamua kuacha”, alisema Rais Kikwete huku akicheka.

Hata hivyo, Raisi Kikwete amewataka Watanzania kutokata tamaa na kufanya vibaya kwa sekta ya michezo na badala yake jitihada za kuendeleza sekta hiyo ziendelee na ipo siku sekta hiyo itafanya vizuri kimataifa.
Katika hatua nyingine Rais Kikwete amesema serikali yake imeingia ubia na makampuni ya kimataifa ya Symbion Power na klabu ya Sunderland ya Uingereza kwa ajili ya kujenga kituo cha michezo kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam ambacho kinategemewa kuanza kazi mwezi Septemba.

Pamoja na hayo, Rais Kikwete amesema serikali yake pia imechukua jitihada za makusudi kuendeleza sekta ta muziki na filamu kwa kuwaalika wataalamu kutoka Marekani kutoa mafunzo ya sekta hizo kwa wasanii wa Tanzania ili wafanye kazi nzuri itakayotambulika kimataifa.

Karibu utangaze nasi sasa wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 80, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.Gharama zetu ni rahisi sana na tangazo lako litawafikia au kutazamwa na zaidi ya watu elfu tisini.

No comments:

Post a Comment