Friday, 3 July 2015

HII NAYO KALI ETI CHINA SI RUHUSA KUPATA UJAUZITO BILA RUHUSA MAALUM!!


Hivi utajisikiaje pale ambapo kampuni yako au ofisini kwako unakofanyia kazi ukaambiwa kuwa hutakiwi kupata ruhusa ya kuanzisha familia hadi pale ofisi itakapoamua?

Sasa huko nchini China kuna Kampuni moja ambayo inapanga kutoa masharti ya namna hiyo kwa wafanyakazi wake kabla ya kuanzisha familia.

Sheria hiyo inawataka wanawake wote walio kwenye ndoa kuwalazimu wawe wamehudumu kwa mwaka mmoja kwenye kampuni hiyo kabla ya kutuma kibali cha kukubaliwa kushika mimba. Huku yeyote atakayekiuka sheria hiyo na kushika mimba atatozwa faini na kunyimwa madaraka yeyote, hata kama amefuzu.

Hata hivyo, Shirika la Utangazaji nchini China limekosoa vikali kampuni hiyo iliyoko mkoa wa Henan na kusema haina ubinadamu kwa wafanyikazi wake.

Pamoja na hayo itakumbukwa kwamba si jambo la ajabu kwa muingiliano wa masuala binafsi nchini China, hasa sheria ya mtoto mmoja iliyowekwa na serikali miaka ya sabini ambayo inawalazimisha wazazi kupata mtoto mmoja pekee.

Kama unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali unaweza kuwasiliana na Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba, 0716 300 200, 0769 400 80, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.
 

No comments:

Post a Comment