Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 9 July 2015

HII NI MAALUM KWA WEWE AMBAYE UNGEPENDA KUJUA HALI YA BURUNDI KWA SASAKufuatia kuwapo kwa machafuko na maandamano nchini Burundi ambayo yalikuwa yakimpinga Rais Pierre Nkurunzinza kuwania muhula wa tatu imelezwa kuwa hali ya utulivu imerejea nchini humo.

Msemaji wa rais Nkurunziza Gervais Abayeho amesema maandamano ya kupinga muhula wa 3 wa rais Nkurunziza yamesitishwa na shule zimefunguliwa na watu kurejea katika kazi zao za kila siku.

Abayeho alisema kuwa kuonekana kwa hali hiyo ni kiashiria tosha kuwa hali ya kawaida imerejea nchini Burundi.

Aidha msemaji huyo, Abayezo alifahamisha kuwa warundi 40,000 waliokuwa wamekimbia nchi hiyo wamerejea nchini mwao ili kuendelea na kazi zao za kila siku, huku wakihitaji kutimiza wajibu wao wa kupiga kura katika uchaguzi wa rais utakaofanyika Julai 15.

Hata hivyo licha ya maandamano kusimama, bado vitendo vya uhalifu vinaripotiwa jijini Bujumbura.

Pamoja na hayo, kuendelea kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na mashirika ya kutoa misaada yalifahamisha kuwa zaidi ya watu 140,000 waliikimbia Burundi wakihofia machafuko baada ya chama tawala kumteuwa rais Nkurunziza kuwania kiti cha urais kwa mara ya 3.

Kama unahitaji kutangaza nasi kupitia tovuti hii, wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 80, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.Gharama zetu ni rahisi sana na tangazo lako litawafikia au kutazamwa na zaidi ya watu elfu tisini.

No comments:

Post a Comment