Thursday, 30 July 2015

HIVI NDIVYO LOWASSA ALIVYOCHUKUWA FOMU YA KUWANIA URAIS KUPITIA CHADEMA


Leo Julai 30, 2015 aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa amefika makao makuu ya CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam na kuchukuwa fomu ya kuwania urais kwa tiketi ya chama hicho.

Mhe.Lowassa amechukua fomu hiyo ikiwa ni siku chache tu tangu alipokihama chama chake cha CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi karibu,jijini Dar es Salaam.

Picha za Mh;Lowassa alipofika makao makuu ya CHADEMA mapema leo jijini Dar es Salaam.


Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa pichani akiwapungia wanachama na wafuasi mbalimbali wa chama cha CHADEMA waliofika kumshuhudia katika zoezi la kuchukua fomu.
Unaweza kutangaza na tovuti hii sasa wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment