Monday, 20 July 2015

HIVI NDIVYO UNAVYOWEZA KUPATA UGONJWA WA KISONONOVijidudu vya kisonono

Magonjwa ya zinaa ni miongoni mwa magonjwa ambayo huwakabili vijana wengi na ni moja ya magonjwa hatari sana.

Leo tutaanza kuzungumzia kwanza ugonjwa wa kisonono, huu ni ugonjwa ambao unasababishwa na vijidudu au bakteria waitwao 'Neisseria gonorrheae.'
Moja ya madhara yanayoweza kutokea endapo mgonjwa wa kisonono hata pata matibabu sahihi ni pamoja na kusababisha ugumba.

Ugonjwa wa kisonono huambukizwa kwa kufanya ngono zembe na mtu mwenye maambukizi tayari.

Ngono hiyo inaweza kuwa ni ngono ya mdomo au ukeni na hata kinyume na maumbile pia, kwa kawaida vijidudu vya ugonjwa huu hukaa kwenye majimaji ya sehemu za siri kama vile majimaji ya ukeni na shahawa.

Majimaji hayo yanapopenya kupitia ngozi laini za sehemu za siri husababisha maambukizi kutokea na ikumbukwe kwamba hata kufanya ngono mara moja na mtu mwenye kisonono huweza kusababisha mtu anapata maambukizi.

Hivyo ndivyo namna maambukizi ya ugonjwa huu ya kisonono ynavyoweza kuenea, endelea kuwa karibu nasi na nitakuleta dalili za ugonjwa, tiba yake na namna ya kujikinga, lakini kwa sasa kama unaswali unaweza kuwasiliana na Dk Abadallah Mandai kwa simu amba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com au ukurasa wa facebook uitwao Mandai Herbalist Clinic - mhc

No comments:

Post a Comment