Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 24 July 2015

HIVI NDIVYO WAKAZI WA MWANZA WALIVYOHAMASIKA KUIPOKEA CHADEMA MWANZA (PICHA)Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wiki hii kililifunika jiji la Mwanza, baada ya kufanya mkutano mkubwa wa hadhara uliokusanya maelfu ya wakazi wa jiji hilo katika viwanja vya Magomeni.

Mkutano huo uliohudhuria na viongozi wote wa juu wa chama hicho pamoja na waliokuwa wabunge wawili wa CCM, James Lembeli (Kahama) na Esther Bulaya (Viti Maalum) waliopokelewa rasmi baada ya kujitoa katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na chama hicho.
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa akihutubia mamia ya wakazi wa Mwanza
Mkutano huo ulikusanya wafuasi kutoka Mwanza na mikoa ya jirani ikiwamo Shinyanga (Kahama) na Mara (Bunda).


Leo nimeona nikupatie baadhi ya picha za mkutano huo


Mbunge wa Viti Maalum Kutoka mkoa wa MARA aliyehamia CHADEMA kutoka CCM Mh Esther Bulaya akihutubia katika mkutano mkubwa jijini Mwanza jana.
Mwenyekiti wa Baraza la wanawake Taifa CHADEMA Mh Halima Mdee akiwa na Mh Esther Bulaya wakiwapungia mamia ya wakazi wa Mwanza waliofika kuwalaki.

Naibu Katibu mkuu wa CHADEMA bara Mh John Mnyika akiwa na Mbunge wa Kahama aliyejiunga na CHADEMA kutoka CCM Mh James Lembeli wakiwapungia mikono wakazi wa Mwanza.
Ikiwa utahitaji kutangaza na tovuti hii unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800 au email dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment