Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 4 July 2015

HIVI UNAJUA KUWA DUNIANI KUNA WANANDOA TAKRIBANI MILIONI 50 HAWANA WATOTO NA WANALIA KILA SIKU NA KUHANGAIKA KUSHIKA MIMBA ILA HAWASHIKI, PATA NAFASI YA KUFAHAMU SABABU KUBWA ZA TATIZO HILO


Asilimia 15% ya wanandoa duniani ambao wanatamani kupata watoto wanakumbwa na matatizo ya uzazi

Kupata watoto katika ndoa ni mchakato wa asili ambao wanandoa huamua wakati wa ndoa yao
Inajulikana tangu kitambo ya kwamba kuwa na watoto huongeza umoja baina ya familia, hukidhi matarajio ya jamii na pia hudumisha na kuendeleza ukoo.

Hata hivyo, sio wanandoa wote ambao wanataka watoto au kupanga kuwa na watoto na wanapata. Idadi ya watu ambao wana matatizo ya kushika mimba ni kubwa katika kipindi hiki. Kwa mujibu wa utafiti uliodhaminiwa na shirika la afya duniani, WHO unafahamisha kuwa kwa sasa takriban wanandoa milioni 50 wanashindwa kupata watoto ingawa wamejaribu zoezi hilo kwa miaka 5.

Asilimia 15% ya wanandoa wote duniani ambao wanatamani kupata watoto wanakumbwa na matatizo ya uzazi. Kitendo cha kushindwa kutunga mimba kwa zaidi ya mwaka kinachambuliwa na wataalam kama tatizo la uzazi.

Hali hii hutokana na sababu mbalimbali ambazo baadhi yake ni rahisi kuzitatua na nyingine ni ngumu kutatuliwa. Kwa mujibu wa uchunguzi, theluthi moja ya matatizo ya uzazi katika familia zote zenye matatizo haya husababishwa na wanaume.

Theluthi nyingine ya matatizo haya huwa katika upande wa wanawake na theluthi ya mwisho huwa ni kutoka kwa wote mwanamke na mwanaume. Kwa mantiki hii, sio rahisi kutambua chanzo cha tatizo na katika ile asilimia 15% ya wanandoa wote ambao hukumbwa na tatizo hili, hawana uhakika kwamba hili tatizo linatıokana na wanaume au wanawake.

Tatizo kubwa la uzazi kwa wanawake ni matatizo ya mayai ya uzazi. Wataalam wanaeleza kwamba uwezo wa msichana huwa katika kiwango kikubwa katika umri kati ya miaka 25 hadi 27 na huanza kupungua baada ya umri wa miaka 32.

Hii inamaanisha kwamba kadri saa yakibiologia inavyozidi kusonga muda wake ndivyo uwezekano wa mwanamke kushika mimba unavyopungua. Kwasababu, umri husababisha idadi na ubora wa mayai ya uzazi kupungua.

Tatizo sio hili tu bali matatizo ya homoni za uzazi, kuziba kwa mirija ya Falopian, kurundikana kwa seli nyingi kwenye mfuko wa uzazi au mapungufu ya kimaumbile husababisha mwanamke kushindwa kushika ujauzito.

Kwa wanaume matatizo ya uzazi husababishwa na uchache wa mwegu za kiume, mwendo-kasi mdogo wa mbegu hizo au kukosekana kabisa kwa nguvu za kiume. Wataalamu wanafahamisha kuwa msongo wa mawazo ndio chanzo kikubwa cha tatizo hili kwa wanaume.

Msongo wa mawazo huathiri tezi na hivyo kushindwa kuzalisha homoni.

Wanandoa ambao wanahitaji kuwa na mtoto wanatakiwa kumuona mshauri au mtaalam endapo watashindwa kupata mtoto ndani ya kipindi cha mwaka mmoja. Watafanyiwa uchunguzi na chanzo cha tatizo lao kitajulikana.

Kisha wataaalam hawa watashauri tiba kulingana na tatizo lilivyo.

Sasa kama umekuwa ukihitaji kupata mtoto kwa muda mrefu na hujafanikiwa kupata, ni vizuri ukafika Mandai Herbalist Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam ili tuweze kukusaidia kuondokana na tatizo hilo kwa kukupatia dawa zetu zitakazokufanya uweze kushika mimba na hatimaye kuitwa mama, ni wengi wameshafanikiwa kupitia dawa zetu. Tupigie simu namba 0716 300 200, 0769 400 80, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment