Friday, 24 July 2015

HIZI NDIZO NJIA ZA KUZUIA HARUFU MBAYA SEHEMU ZA SIRI


Tatizo la kutoa harufu sehemu za siri kwa wanawake ni moja ya shida ambayo huwakwaza wanawake wengi na kufanya kukosa raha kabisa katika maisha yao.Lakini hapa leo kuna haya mambo kadhaa ambayo yanaweza kuwa msaada kwako wewe mwanamke ambaye unasumbuliwa na tatizo hilo.


Kwanza kabisa jenga utaratibu wa kuosha uke wako kwa maji safi na salama kila unapomaliza kujisaidia haja ndogo, baadhi ya wanawake wengi huwa hawana mazoea na utaratibu wa kujisafisha mara baada ya haja ndogo, licha ya kwamba huu ni utaratibu muhimu sana katika maisha ya kila siku ya mwanamke.


Kumbuka kwamba unapokuwa unajisaidia haja ndogo yako inapotoka lazima kutakuwa na mabaki kidogo yatabaki kwenye mashavu ya sehemu zako za siri. Hivyo hayo mabaki baada ya muda yatachanganyikana na jasho na kisha kutengeneza harufu mbaya ndio maana inaimizwa kujisafisha kila unapomaliza kujisaidia haja ndogo.


Jambo linguine la msingi katika kuepuka tatizo hili ni kuvaa nguo za ndani zenye asili ya pamba, hii ni kwa sababu pamba huwa na uwezo wa kupitisha hewa na sehemu za siri za mwanamke huhitaji hewa inayoingia na kutoka. Hata kama hewa inaingia kwa kiasi kidogo bado itasaidia kufanya sehemu hizo za siri kuwa katika hali nzuri.


Pia punguza kuvaa nguo zenye kubana sana muda wote, kwasababu nguo za kubana husababisha majasho sehemu za siri na hivyo kuchangia sehemu hizo kutoa harufu pia.
Usivae nguo ya ndani moja siku nzima, kutokana na maumbile ya mwanamke yalivyo, mwanamke anapaswa kubadili nguo ya ndani mara mbili au tatu kwa siku.


Badili pads zako mara kwa mara unapokuwa kwenye siku zako, unapobadili pads mara kwa mara itakusaidia kuwa na amani na kuzuia bacteria kujikusanya na hivyo kuzuia kutoa harufu mbaya sehemu zako za siri.


Hakikisha unanyoa nywele zako za sehemu zako za siri mara kwa mara kwa sababu nywele hizo zinapokuwa ndefu hutengeneza maficho ya kila aina ya uchafu ikiwa ni pamoja na jasho pamoja na majimaji yanayokutoka ukeni nay ale mabaki ya haja ndogo.


Osha sehemu zako za siri kwa kutoka mbele kurudi nyuma, wakati uanajisafisha unapopeleka mkono nyuma unakuwa kama unazoa bacteria na uchafu kwenye uke, na huo ndio utakuwa mwanzo wa sehemu hiyo ya siri kuanza kutoa harufu mbaya.

  Unaweza kuwasiliana nasi Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkamandaitz@gmail.com ili kupata huduma zetu, kumbuka kuwa tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment