Monday, 6 July 2015

HUU NDIO UAMUZI WA RAIS KENYATTA KUHUSU POMBE HARAMU NCHINI MWAKE


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, ameanzisha kampeni ya siku tatu kwa ajili ya kupiga vita uuzaji wa pombe haramu katika mji mkuu wa Nairobi na mkoa wa kati.

Aidha, kampeni hiyo imelenga kufutilia mbali vibali vya wamiliki wa vilabu vya pombe haramu na kuharibu bidhaa zao zilizopigwa marufuku.

Akitoa maelezo Ikulu, rais Kenyatta aliwafananisha wauzaji wa pombe haramu kama ‘‘wamachinga wa mauti.’’

Mbali na hayo Rais Kenyatta pia aliamuru wabunge kufanya misako katika maeneo yao wanayowakilisha ili kutekeleza kampeni hiyo.

Jinsi kampeni hiyo ilivyokwenda
Itakumbukwa mnamo mwezi Mei, zaidi ya watu 60 walipoteza maisha na wengine zaidi ya 20 wakafikishwa hospitalini baada ya kuathirika kwa unywaji wa pombe haramu katika mkoa wa kati nchini Kenya.

Wengi wa walevi hao waliopona wanaarifiwa kupofuka macho kutokana na kemikali hatari zilizokuwa ndani ya pombe haramu.

 Kama unahitaji kutangaza nasi kupitia tovuti hii, wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 80, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.Gharama zetu ni rahisi sana na tangazo lako litawafikia au kutazamwa na zaidi ya watu elfu themanini

No comments:

Post a Comment