Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 24 July 2015

HUU NDIO UGONJWA WA ZINAA AMBAO MADHARA YAKE NI MAKUBWA HADI KWENYE MOYO NA UBONGO


Ugonjwa wa kaswende ni ugonjwa wa zinaa, ambao husababishwa na vijududu vya bakteria viitwavyo Treponema pallidum.

Nii kati ya magonjwa ya zinaa ambayo yapo kwa sana na yana hatari ya kuathiri moyo na ubongo kama mtu asipopata matibabu kamili.

Ugonjwa huu huweza kutibika na kupona kabisa endapo utapata tiba sahihi kama ilivyo kwa magonjwa mengine ya ngono.

Ugonjwa huu wa kaswende huambukiza kwa njia ya ngono, hii inaweza kuwa kwa ngono za ukeni, mdomoni au kinyume na maumbile. Kwa hiyo mtu anaweza pata kaswende kwenye sehemu za siri, hata mdomoni.

Halikadharika ugonjwa huu pia huweza kuambukizwa kwa njia ya kuongezewa damu ya mtu mwenye kaswende au kutoka kwa mama mjamzito mwenye kaswende kwenda kwa mtoto wake tumboni.

Mara nyingi mtu hupata dalili za kaswende siku 9 mpaka 90 toka alipopata vijidudu vya ugonjwa huu na dalili zake hutegemea na hatua ya ugonjwa. Hivyo baadhi ya wagonjwa wanaweza wasioneshe dalili ingawa wamepata maambukizi.

Miongoni mwa dalili za ugonjwa huu ni pamoja na kutoka na kipele/vipele sehemu za siri kisicho na maumivu, halafu hupasuka kutengeneza kidonda ambacho hakiumi. Kidonda hiki hupona ndani ya wiki 2 -6 kama mtu hajatibiwa na endapo mtu hakupata matibabu, dalili hizi hupona lakini vijidudu vya kaswende bado huendelea kuwa ndani ya mwili na kuendelea hatua ya pili ya ugonjwa wa kaswende (secondary syphilis).

Mgonjwa pia huweza kuwa na homa sambamba na kujisikia vibaya na kichwa kuuma ikiambata na vipele kwenye mwili na mikono ambavyo haviwashi. Pia vipele vingi huweza kutokea sehemu za siri.

Hatua ya tatu ya kaswende (tertiary syphilis) ambayo ni mbaya zaidi hii huanza kushambulia sehemu mbalimbali za mwili hasa mishipa ya damu na moyo na ubongo. Hii hutokea miaka 3 -10 baada ya kupata maambukizi ya vijududu vya kisono.

Kama utakuwa umekuwa ukisumbuliwa na magonjwa ya zinaa kwa muda mrefu au kuna dalili za ugonjwa huo au ugonjwa wowote ule ni vyema ukawasiliana nasi Mandai Herbalist Clinic ili upate msaada kutoka kwa Tabibu Abdallaha Mandai na utapata tiba nzuri na kupona kabiasa ili kuepuka madhara ya magonjwa haya ya zinaa.

Unaweza kuwasiliana na Tabibu Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800 au 0784 300 300 barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment