Tuesday, 28 July 2015

IFAHAMU HII RANGI YA UKUTANI YENYE UWEZO WA KUKOMESHA TABIA YA KUKOJOA KWENYE KUTA ZA NYUMBA


Kama wewe ni miongoni mwa wale watu ambao hukojoa mitaani hovyo hasa kwenye ukuta basi kuna hii dawa yako ambayo itakomesha tabia hiyo.

Sasa huko California kwenye mji wa San Francisco unaambiwa kuwa kitendo cha wewe kukojoa tu ukutani basi huenda mkojo ukakurudia mwenyewe.

Mmoja wa ajenti wa wizara ya nguvu kazi mjini humo amesema kuwa wanajaribu kuanza kutumia aina ya rangi ya ukuta inayorudisha mkojo hivyo mtu yeyote atakaye tumia ukuta uliopakwa rangi hiyo, mkojo wake utakuwa ukimrudia, hiyo ni kwa mujibu wa msemaji wa mawakala hao. Ambapo ameeleza kuwa rangi hiyo itapakwa katika maeneo ambayo ni maarufu kwa watu kujisaidia ovyo ovyo.

Rangi hiyo inayojulikana kama Ultra-Ever Dry inatengeza kizuizi cha hewa mbele ya ukuta huo ambao utafanya mkojo na aina yoyote ya maji kugonga na kurudi, maelezo hayo ni kwa mujibu wa watengezaji wa rangi hiyo. Pia wamesema kuwa wamepata simu nyingi kutoka kwa watu wanaotaka wapakiwe rangi hizo kwenye majengo yao maeneo jirani, Alisema Gordon.

Rangi hiyo maalum ikipakwa kwenye baadhi ya kuta ili kukomesha taibia hiyo
Katika majaribio ya mradi huo, mamlaka ya San Francisco ilipaka rangi kuta 9 zilizo karibu na maeneo ya burudani na makazi ya watu wasio na nyumba, huku maandishi yaliondikwa kwa lugha ya kiingereza, kichina na kihispania kwenye kuta hizo yakisema, shikilia kwanza , tafuta usaidizi mahali pengine.

Mkurugenzi wa mawakala hao alipata wazo hilo baada ya kupata maarifa kuhusu rangi hiyo akiwa katika sehemu moja ya burudani nchini Ujerumani.

Endelea kuwa karibu na tovuti hii kwa taarifa zaidi kila siku, lakini pia unaweza kutangaza nasi kwa gharama nafuu sana tupigie simu namba 0716 300 200, 0784 300 300

No comments:

Post a Comment