Friday, 17 July 2015

IFAHAMU HII TIBA YA KICHOMI KWA KUTUMIA KITUNGUU SWAUMU


Mara nyingi watu wengi hulalamika sana kusumbuliwa na tatizo la kichomi ambalo husababishwa na hitilafu katika mapafu na chanzo cha hitilifa hizo huweza kuwa mashambulizi ya vijidudu mfano ‘steptococcus’ ‘preumococcus’ na ‘staphylococcus’ mashambulizi ya virusi, matatizo ya ukungu, matatizo ya minyoo, kuvuta hewa yenye sumu.

Mara nyingi matokeo ya matatizo haya huwa ni homa kali, maumivu makali kifuani, kupumua kwa shida, wakati mwingine ikifuatiwa na kikohozi chenye makohozi.
Moja ya tiba nzuri za kichomi ni pamoja na kitunguu swaumu, karoti, spinachi na tango.


Unapotumia kitunguu swaumu unapaswa kuponda punje kumi za kitunguu swaumu hadi ziwe katika hali ya uji uji kisha paka kitunguu hicho sehemu za kifua zenye maumivu. Fanya hivyo asubuhi na jioni kwa muda wa siku saba.

Kama ungehitaji kutumia tiba hii ni vyema ukafanya mawasiliano nasi Mandai Herbalist Clinic ili kupata maelekezo zaidi. Tupigie simu namba 0716 300 200, 0769 400 300, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment