Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 2 July 2015

IFAHAMU NCHI AMBAYO IMETHIBITISHWA KUFANIKIWA KUZUIA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO.


Inafahamika wazi kuwa ugonjwa wa Ukimwi ni ugonjwa ambao umeenea karibu duniani kote na mataifa mbalimbali yamekuwa yakipambana katika kupunguza idadi ya watu kuambukizwa ugonjwa huu,  jambo ambalo pia limekuwa na ugumu wake kiasi huenda kutoka na njia za maambukizi za ugonjwa huu.

Lakini hii leo nimeipata hii taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) ambapo wamethibitisha kuwa nchi ya Cuba imemaliza kabisa maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama mzazi kwneda kwa mtoto.

Mafanikio hayo yameelezwa kufanikiwa kufuatia kampeni ya muda mrefu miongoni mwa wanawake wajawazito, ambao wamekuwa wakishauriwa kuanza kupokea matibabu mapema na kufanyiwa vipimo mahususi ili kujua hali ya afya zao wakati wote wa kipindi cha ujauzito .

Mkuu wa WHO, Daktari Margaret Chan, ametaja ufanisi huo kuwa ''ni mkubwa zaidi kuwahi kutokea kwa afya ya umma.''

Kwa mujibu wa takwimu za WHO, Kila mwaka takribani wanawake milioni 1.4 walioambukizwa virusi vya Ukimwi duniani, hupata ujauzito na pale wanapokosa matibabu ya mapema asilimia 15 hadi 45 ya wanawake hao huwaambukiza watoto wanaojifungua wakati wa kujifungua na kupitia kwenye maziwa ya mama. 

Pia imeelezwa kuwa kote duniani wanawake 7 kati ya 10 ambao wameambukizwa virusi vya Ukimwi hupokea madawa ya kupunguza makali ya Ukimwi kwa lengo la kuzuia maambukizi kwa watoto watakaojifungua.

Naye Dk. Carissa Etienne, ambaye amekuwa akishirikiana na WHO amesema kuwa mafanikio ya Cuba yanapaswa kuigwa kote duniani ili kupunguza au hata kumaliza kabisa maambukizi ya Ukimwi na kaswende kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto.

Kama unahitaji kutangaza nasi kupitia tovuti hii, wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 80, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.Gharama zetu ni rahisi sana na tangazo lako litawafikia au kutazamwa na zaidi ya watu elfu themanini

No comments:

Post a Comment