Tuesday, 28 July 2015

ILIKUWA KAMA TETESI VILE LAKINI SASA NI LIVE LOWASSA RASMI NDANI YA UKAWA

Ilikuwa kama tetesi tu kuhusu aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa kukihama chama chake cha Mapinduzi CCM kuhamia UKAWA, lakini sasa si tetesi tena maana James Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR - Mageuzi jana aliweka bayana kuhusu ishu hii.

Maamuzi hayo yalifuatiwa baada ya Mkutano Mkuu kufanyika Makao Makuu ya CUF na kutoka na majibu ya kuamua kumkaribisha Lowassa ndani ya Umoja huo.

Akimualika Lowassa, Mbatia amaesema kuwa “UKAWA tunahitaji Viongozi wenye sifa, uwezo na weledi katika kulinda, kuheshimu na kusimamia rasilimali za Taifa kwa maslahi ya Taifa.. Nachukua fursa hii kumualika Mheshimiwa Lowassa ajiunge na UKAWA na tuko tayari kushirikiana nae kuiondoa CCM madarakani" 

Katika hatua nyingine Mh;Mbatia amesema kuwa “Uchaguzi wa October 2015 ni fursa ya kipekee ya kuleta mabadiliko katika nchi yetu kuondoa ukandamizi uliojikita CCM. Watanzania wanahitaji Mabadiliko yenye fikra mpya na bunifu kwa maslahi ya Watanzania wote“

Msikilize hapa Mheshimiwa Mbatia akimkaribisha Lowassa ndani ya UKAWA, Bonyeza 'Play' hapo chini kusikiliza>>>Kama unahitaji kutangaza tukio lako au biashara unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300 barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment