Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 3 July 2015

ISHU YA KUKATWA MUDA WA HEWANI KWENYE SIMU ILIPATA NAFASI YAKUZUNGUMZWA JANA BUNGENI, MAJIBU YAKE YAPO HAPA

Je, ni mara ngapi umewahi kuweka vocha kwenye simu yako halafu baadaye ukakuta ile hela uliyoweka haipo, ingawaje hukuitumia kwa kupiga simu wala kutuma sms?

Naamini wengi tumeshawahi kukutwa na hali hiyo, sasa moja ya mambo ambayo yalipata nafasi ya kusikika bungeni ni pamoja na hili, ambapo Mbunge Murtaza Mangungu aliuliza swali hili 'Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba wanapoteza pesa kujiunga na vifurushi ama wanaponunua vocha. Serikali itachukua hatua gani kudhibiti Makampuni ya simu ambayo yanafanya wizi kwa wananchi”

Majibu ya swali hilo yalitolewa na Naibu Waziri Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, January Makamba, ambapo alisema kuwa 'Serikali imetoa onyo kwa TCRA kwamba tunataka hatua zianze kuchukuliwa na namna mpya ikiwemo kuhakikisha kwamba kuna kituo ambacho kipo saa zote kwa ajili ya kupokea simu na malalamiko ya watu na ni rahisi kituo hicho kufikika na watu wanahakikishiwa majibu, malalamiko yasiposhughulikiwa ndani ya saa 48 hatua za Kisheria zinachukuliwa kwa makampuni ya simu”

Unaweza kumsikiliza hapa chini Waziri Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, January Makamba, akijibu swali hilo. Bonyeza 'Play'
Kama unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali unaweza kuwasiliana na Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba, 0716 300 200, 0769 400 80, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment