Tuesday, 28 July 2015

JE, HALI YA UNENE KUPITA KIASI HUWEZA KUSABABISHIA MATATIZO YA HEDHI?


Mara nyingi tumekuwa tukipokea maswali kutoka kwa wafuatiliaji wetu mbalimbali ambao huuliza maswali yao kupitia mitandao yetu ya kijamii, leo nimeona tujibu hili swali moja la Maimuna K.

Yeye swali lake lilitufikia likiwa hivi “ Naitwa Maimuna K. Mimi ni mnene na siku zangu za hedhi hubadilika mara kwa mara je, unene unaweza kuwa sababu?

Hivyo napenda kujibu swali hili kwa faida ya Maimuna, lakini pia na wasomaji wetu wengine, majibu ni kwamba ni kweli wanawake wengine hukumbwa na tatizo hilo kutokana na unene.

Imethibitika kuwa na uzito mkubwa kwa wanawake huweza kuchangia kuingia katika hatua za kuacha kupata hedhi kwa kuchelewa kwa mwaka mmoja zaidi ikilinganishwa na wanawake ambao hawana uzito mkubwa .

Kitaalamu hali hiyo inatokana na uingiliaji wa mafuta kwa watu wanene au walio na uzito uliopitiliza na homoni za kujamiiana yaani 'sex hormones', lakini pia uvutaji wa sigara huweza kuwa sababu ya hili.

Tatizo lingine ni kwamba wanawake wanaovuta sigara baadhi yao hukosa hedhi au kuharakisha kutopata hedhi miaka miwili kabla ya wakati au umri wa miili yao kufanya hivyo.

Pia wanawake walevi wa pombe yaani wanaokunywa pombe kila siku nao wapo kwenye hatari ya kukubwa na tatizo hili, lakini walio katika hatari zaidi ni wale wenye umri kati ya miaka 25 na 49, hawa wanaweza kufunga hedhi kama wataendelea na tabia hiyo ya unywaji wa pombe kila siku.
Pia na wewe unaweza kuuliza maswali yako kupitia inbox yetu ya Facebook ukurasa unaitwa Mandai Herbalist Clinic- mhc au kwenye email ya dkmandaitz@gamail.com kisha utakuwa ukipata majibu yako kupitia website hii, lakini pia unaweza kutupigia simu 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800

No comments:

Post a Comment