Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 15 July 2015

JESHI LA POLISI LATAKAZA DONGE NONO KWA AMBAYE ATATOA TAARIFA ZA KUFANIKISHA KUPATIKANA KWA WALIOVAMIA KITUO CHA POLISI STAKISHARI

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova
Kufuatia tukio la kuuawa kwa watu saba wakiwemo askari wanne katika Kituo cha Polisi Stakishari, Ukonga jijini Dar es Salaam, Jeshi la Polisi nchini limetangaza donge nono la Shilingi milioni 50 kwa watakaofanikisha kukamatwa kwa wahusika wa tukio hilo.

Akizungumza jana ofisini kwake, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova alisema, yeyote atakayetoa taarifa za wahalifu hao atazawadiwa kitita hicho huku ikibaki kuwa ni siri kati ya Polisi na mtoa taarifa.

Aidha, alisema kutokana na tukio hilo, kuna mpango wa kuweka kamera za usalama katika vituo vya Polisi, ili kuweka kumbukumbu za watu wanaoingia na kutoka hata kama ni wahalifu iwe rahisi kupatikana.

“Tumeona ni bora kuongeza kiwango cha tahadhari na ulinzi katika vituo vya Polisi na maeneo mengine. Kwa hiyo mtu asije akaenda kituoni akashangaa kuona anachukua muda mrefu kuhudumiwa na anakaguliwa sana, hiyo kwa sasa ni kawaida,” alisema Kova.

Hata hivyo Kamishina Kova alisema, Jeshi la Polisi limekubaliana kutotoa taarifa ambazo baadhi yake zinaweza kuleta hamaki kwa wananchi, kwani lengo siyo kuwatisha wananchi bali kushirikiana nao na kuhakikisha kuwa wahalifu na silaha zilizoporwa zinapatikana.

“Unajua unaweza ukasema labda zimeibwa silaha na mabomu ukawapa hofu wananchi kwa kudhani hawako salama, hivyo tumeona siyo kila taarifa ni ya kuiweka wazi ili kuweka tahadhari kwa wananchi,” alisema.

Mtu yeyote atakayekuwa na taarifa awasiliane na yeye mwenye kwa namba 0754 034 224, Msemaji wa Polisi Advera Bulimba 0713 631 667 na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Diwani Athuman kwa namba 0715 323 444 au kuonana na viongozi wa makao makuu ya Polisi na Kanda Maalumu ana kwa ana.

Pamoja na kutolewa kwa kiasi hicho cha fedha kumeelezwa kunakwenda sambamba na dhana ya Polisi Jamii na ulinzi shirikishi, hivyo kumfanya Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Ernest Mangu kuagiza wananchi washirikishwe katika suala hilo linalohusu ulinzi na usalama wa mali zao na Watanzania kwa ujumla

Itakumbukwa kuwa mbali na mauaji hayo, watu waliovamia kituo hicho walivunja ghala la silaha na kupora bunduki za kivita ambazo idadi yake haijafahamika, lakini ikikisiwa kuwa ni zaidi ya 15.

Halikadhalika Kamanda Kova alitaka wananchi wasiwe na hofu na Jeshi la Polisi kwa kudhani limelegea, bali watoe ushirikiano kwa taarifa ili wahalifu hao waweze kutiwa mbaroni.Kama unasumbuliwa na tatizo la fangasi sehemu za siri na ungependa kuanza kutumia dawa zetu ili kupona kabisa basi tutatafute Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300 au 0769 400 800

No comments:

Post a Comment