Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 24 July 2015

JIKINGE NA FANGASI ZA SEHEMU ZA SIRI KWA NJIA HIZI


Magonjwa ya faangasi za ukeni husababishwa na fangasi aina ya Candida albicans na ni kati ya magonjwa ambayo husumbua wanawake mara kwa mara.

Ugonjwa huu huweza kueneza au kuambukizwa kutokana na matumizi ya vyoo vichafu pamoja na kuchangia nguo za ndani na mataulo.

Hali ya joto, na unyevunyevu mwingi na kuvaa nguo za kubana huchangia pia kutokea kwa fangasi ukeni. Ugonjwa huu unaweza kuambukizwa kwa njia ya ngono, ingawa sio kwa kiasi kikubwa.

Tatizo hili pia huwa linakuja na dalili zake miongoni mwa daluili zake ni pamoja na kuwashwa sehemu za siri hasa kwenye uke na mashavu ya uke, kutokwa na maji maji meupe mfano wa maziwa kutoka kwenye uke ambayo hayana harufu mbaya wengine huweza maumivu wakati wa kukojoa kwa baadhi ya wagonjwa. Mara chache hali hii hutokea, ikisabaishwa nakuchubuka wakati wa kujiwasha.

Lakini ili kujikinga na ugonjwa huu ni vyema kuzingatia usafi wa nguo za ndani na kuvaa nguo za ndani zilizokauka vizuri. Epuka zenye unyevunyevu au mbichi, usafi wa choo na usafi wa sehemu za siri na kujikausha vizuri.

 Unaweza kuwasiliana nasi Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkamandaitz@gmail.com ili kupata huduma zetu, kumbuka kuwa tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment