Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 15 July 2015

JOTO LA SIASA BADO LINAENDELEA SASA NI ZAMU YA KUCHUKUA FOMU KWA WATAKA UBUNGE NA UDIWANI CCM

Ikiwa ni siku chache tu baada ya mchuano wa kuwania uteuzi wa kugombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM uliomalizika kwa Dk. John Magufuli kuibuka mshindi.

Chama cha Mapinduzi CCM sasa kinatarajiwa kuhamia kwa makada wa chama hicho wanaowania kuteuliwa kuwania ubunge na udiwani kote nchini.

Chama hicho tawala, kinatarajiwa kuanza kutoa fomu za ubunge, udiwani na wagombea wa Ujumbe katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Kutokana na kufunguliwa kwa pazia hilo, wananchi wenye sifa za uongozi wamehamasishwa kujitokeza.

Pamoja na hayo kwa mujibu wa ratiba ya mchakato wa uteuzi ndani ya CCM, fomu hizo zitagharimu shilingi 100,000 kwa wagombea wa ubunge na shilingi 10,000 kwa upande wa madiwani, zitatolewa hadi Julai 19, mwaka huu.
Karibu utangaze nasi sasa wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.Gharama zetu ni rahisi sana na tangazo lako litawafikia au kutazamwa na zaidi ya watu elfu tisini.

No comments:

Post a Comment