Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 9 July 2015

KAMA ULIKUWA HAUFAHAMU UMUHIMU WA UKWAJU KATIKA TIBA, BASI HII NI NAFASI YAKO YAKUFAHAMU LEO SOMA HAPA


Ukwaju ni tunda linalotokana na mkwaju, mkwaju ni mti unaotoa matunda ambayo yanajulikana kama ukwaju ambayo wengi huyatumia kwa kula au kutengenezea juisi.

Dk Abdallah Mandai yeye ni mtaalam wa tiba asili hapa nchini anasema mti wa ukwaju unafaida kuanzia mizizi, magome, majani, na hata matunda yake pia,

“Tukianza mizizi ya mkwaju ikitengenezwa vizuri huwa na uwezo wa kutibu magonjwa mengi likiwemo tatizo la mkojo mchafu (UTI)” alisema Dk Mandai

Pia Dk Mandai anabainisha kuwa mizizi inasaidia sana kuzibua mirija ya uzazi, lakini pia humpunguzia mwanamke maumivu wakati wa hedha au wakati wa tendo la ndoa.

Aidha, anafafanua kuwa majani ya mkwaju yanapoandaliwa vizuri husaidia sana kuzuia homa za mara kwa mara ukiwemo ugonjwa wa malaria, kuharisha damu, homa ya matumbo pamoja na vidonda vya tumbo.


Hali kadhalika, majani ya mkwaju yanapokaushwa kivulini kisha kupondwa na unga wake ukichanganywa na mafuta ya nazi husaidia kuondoa magonjwa ya ngozi na mwasho.

“Kwa wenye matatizo ya miguu kufa ganzi au kuwaka moto wachanganye unga wa majani ya ukwaju na mafuta ya nazi kisha mgonjwa achue eneo husika maumivu yanaondoka kabisa,” alisema Dk Mandai.

Ukwaju
Mbali na faida hizo, lakini pia unga huo wa majani ya ukwaju husaidia sana kwa wale wenye matatizo ya pumu (athama), ambapo mgonjwa anapaswa kuchanganya unga huo pamoja na asali kisha mgonjwa anatakiwa alambe husaidia sana kuondokana na hali hiyo pamoja na kifua kikavu.

Sambamba na hayo, Dk Mandai anasema kwamba “ nashauri kuwa mtu atumia juisi ya ukwaju daima angalau anywe mara mbili au hata tatu kwa siku . Kwanza inaongeza vitamin A, B na C, lakini pia ina madini ya chuma, ‘calcium’ na ‘zink’. Pia kwa wale wenye shida ya kupata choo au tumbo kuunguruma ni vizuri wakatumia juisi hiyo itawasaidia kuondokana na matatizo hayo.

Hizo ni baadhi tu ya faida chache za mkwaju, hivyo kutokana na hayo machache, kama unahitaji kufahamu zaidi kuhusu ukwaju au unasumbuliwa na ugonjwa wowote sugu wasiliana na Dk. Abdallah Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment