Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 4 July 2015

KAMA UNASUMBULIWA NA MAUMIVU YA VIUNGO FANYA HAYA ILI KUMALIZANA NA TATIZO HILO


Habari za Jumamosi hii mdau wa www.dkmandai.com karibu katika muendelezo wetu wa kupeana taarifa mbalimbali kuhusu masuala ya afya.

Leo nimeona ni vyema tufahamishane hizi njia zitakazoweza kukusaidia kupunguza maumivu ya viungo, hii ni kutokana na wadau wetu wengi kuomba tulizungumzie suala hili, lakini huenda na wewe leo umeamka ukijihisi maumivu kwenye viungo vyako sasa twende tujue hapa namna ya kufanya.

Ukweli ni kwamba haya maumivu ya viungo ni moja ya tatizo ambalo huwasumbua watu wengi katika jamii hususani wazee.

Sasa ili kumaliza tatizo hilo unaweza kutumia muarobaini pamoja na mdalasini.

Kwa muarobaini unatakiwa kuandaa majani ya muarobaini kisha yatwange na kuyakamua ili kupata juisi yake kiasi cha glasi moja. Kisha utachanganya glasi hiyo na maji ya kunywa glasi saba na utumie mchanganyiko huo kutwa nzima hadi pale yatakapoisha. Fanya hivyo siku kumi hadi kumi na tano.

Ikiwa utahitaji kutumia mdalasini basi utatakiwa kuchemsha mdalasini na maji glasi nane kisha yaache yapoe , kisha kunywa taratibu kwa kutwa nzima. Tumia tiba hiyo kwa siku kumi hadi kumi na tano na baadaye utaanza kuona mabadiliko.

Pia unaweza kufika kwetu Mandai Herbal Clinic tukakupatia dawa nzuri ambayo itakusaidia kumaliza kabisa tatizo hilo. Jambo zuri zaidi kuhusu dawa zetu ni kwamba zimetengenezwa kwa mchanganyiko wa mimea asilia ambayo husaidia kuondosha tatizo hilo kabisa.

Tunapatikana Ukonga, Mombasa jijini Dar es Salaam. Au wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo: 0716 300 200, 0769 400 80, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment