Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 13 July 2015

KAMA UNGEPENDA KUJUA WASIFU WA DK. MAGUFULI SOMA HAPA


Mgombea wa urais wa Chama cha Mapinduzi CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2015 ni Daktari John Pombe Joseph Magufuli, ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Chato lililoko mkoa wa Geita.

Magufuli pia ni Waziri wa ujenzi wa Tanzania na alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1959 wilayani Chato Mkoani Kagera.

Kuhusu elimu yake, Dkt. Magufuli ana Stashahada ya elimu ya sayansi akibobea kwenye masomo ya Kemia na Hisabati, lakini pia ana shahada ya umahiri wa sayansi na shahada ya uzamivu ya kemia.

Aidha daktari Magufuli amewahi kufundisha katika shule ya sekondari Sengerema miaka ya themanini kisha akajiunga na mafunzo ya JKT na alianza siasa mwaka 1995.

Dkt. Magufuli pia amewahi kufanya kazi katika kiwanda cha ‘Nyanza Cooperative Union akiwa Mkemia na baadaye kuondoka hapo na kuwania ubunge.

Magufuli alianza mbio za ubunge mwaka 1995 katika jimbo la Chato na kushinda kisha akateuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuwa naibu waziri wa Miundombinu.Katika uchaguzi wa mwaka wa 2000 pia aligombea ubunge na kushinda na Rais Mkapa akamteua tena kuwa waziri wa miundombinu.

Katika uchaguzi wa mwaka 2005 daktari Magufuli aligombea ubunge kwa mara ya tatu na kupita bila kupingwa.

Katika awamu ya Mh. Rais Jakaya Kikwete alimteua Dkt. Magufuli kuongoza wizara ya Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi na baadaye akamhamishia hadi wizara ya mifugo na uvuvi.

Mwaka 2010 alichaguliwa kuwa mbunge kwa mara ya nne na Rais Kikwete alimrudisha katika Wizara ya Miundombinu na Ujenzi.

Daktari Magufuli anachukuliwa kuwa ni mwanasiasa mwenye msimamo thabiti, mchapa kazi na asiye yumbishwa au hata kufuata upepo wa kisaisa.

Pia Dkt Magufuli anatambulika zaidi kwa Watanzania kwa usimamizi na ujenzi wa barabara na majengo thabiti. Halikadhalika anakumbukwa kwa kuchukua hatua za kutoa amri za kubomolewa kwa majengo ya kifahari ambayo alihisi yalikiuka sheria za ujenzi.

No comments:

Post a Comment