Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 10 July 2015

KAULI YA RAIS KIKWETE KUHUSU HALI YA JESHI, MATUKIO YA UHARIFU NA AJALI ZA BARABARANI


Rais Jakaya Mrisho Kikwete
Rais Jakaya Kikwete jana amehutubia Bunge la kumi kwa mara ya mwisho na alitangaza kuwa Bunge hilo litavunjwa rasmi mwezi Agosti tarehe 20.

Miongoni mwa mengi alyozungumza ni pamoja ni pamoja na kuimarisha Jeshi kwa zana na vifaa vya kisasa na vya kivita, lakini pia na kimafunzo.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa “tumeboresha maslai ya wanajeshi wetu, makazi ya wanajeshi wetu kwa kujenga nyumba mpya za kuishi, utekelezaji wa mpango wa kuwajengea nyumba 10,000 unaendelea vizuri hadi sasa, ujenzi wa nyumba 6064 zinaendelea kujengwa nchi nzima na nyumba 3096 zimekamilika.

Rais Kikwete baada ya kuyasema hayo alisema kuwa "namaliza kipindi changu cha kuwa Rais na Amili Jeshi Mkuu w Majeshi ya Ulinzi na Usalam kwa kujiamini kwamba tupo vizuri."
Pamoja na hayo, Rais Kikwete amesema kuwa mpango wa maendeleo wa kuimarisha jeshi lazima uendelee ili kulifikisha jeshi pale panapokusudiwa.

Pia katika miaka kumi ya utawala wake Rais Kikwete amesema jitihada kubwa za kupambana na uharifu zimefanyika kwa kiasi kikubwa na huku akitoa pongezi kubwa na nyingi kwa Jeshi la Polisi.

Kuhusu matukio ya ajali za barabarani Rais Kikwete alikiri wazi kuwa hilo bado halijafanikiwa kiasi cha kutosha.

"Jambo ambalo hatujafanikiwa vya kutosha ni kupunguza ajali za barabarani, lazima tuendelee kulitafutia muarobaini wake" alisema Rais Kikwete.

No comments:

Post a Comment